Tunasonga mbele na waliyo tayari na sasa kileleni tunaelekea

Darasa la ujasiriamali likiwa linakelekea mwisho kabisa ili kuwapata wajasiramali 10 walio fanya vizuri katika kuandika andiko la bishara. Walimu na wataalamu wa biashara wanafanya jitihada za kila hali kuhakikisha wanafunzi wanakuwa wajasiriamali kweli waliofunzwa na kuelewa mbinu za kuwa wajasiriamali ambao wataweza kukabiliana na changamoto katika biashara zao.

Darasa hili la ujasiriamali lilianzia chuoni JRIIT, ambapo jumla walikuwa wanafunzi 145, lakini mpaka sasa tunaendelea na wanafunzi 20 ambao wameonesha nia ya kuwa wajariamali, pia katika hawa 10 bado watachujwa kulingana na ubora wa andiko lao la biashara (business plan)  ambazo wamekuwa wakifundishwa kuandika.

Kuna vijana ambao walianza darasa bila hata wazo la biashara lakini mpaka sasa wameshapata wazo na kuanza kujaribisha biashara. Vijana wameweza kujiamini na kusimama mbele ya watu kuelezea biashara zao, pia kuweza kuelezea mpango wa fedha wa mwaka mzima katika biashara zao ambazo wengine wameanza na wengine wanatarajia kuanza,